TOBOA NA KIKOBA
SWALI: TOBOA NA KIKOBA NI NINI?
JIBU: Toboa na kikoba ni kampeni inayoelezea huduma za vikundi kidigitali inayo tolewa na benki ya kibiashara Tanzania (Tanzania Commercial Bank Plc.) Huduma hii inaletwa na TCB kwa kushirikiana na mitandao yote ya simu Tanzania, ambapo kwa sasa wateja wanaweza kuendesha shughuli za vikundi vya familia, marafiki, VIKOBA, VSLA, YSLA, ujirani mwema, SACCOS n.k kwa kupitia simu za mikononi huku wakifurahia faida lukuki ikiwa ni pamoja na; i ii iii iv
. Usalama wa fedha za kikundi, . Uwazi,
. Gharama nafuu na,
. Urahisi wa kutumia
SWALI: NI WATEJA WA AINA GANI WATANUFAIKA NA TOBOA NA KIKOBA?
JIBU: Watanzania wote wananufaika na huduma hii bila kujali mitandao yao ya simu.
Hata wale wasio wateja wa TCB, wananufaika na huduma hii ya vikoba kidigitali.
SWALI: HUDUMA YA VIKOBA KIDIGITALI INAPATIKANAJE?
JIBU: Viongozi wa kikundi kwa kushirikiana na wanachama, watachagua mtandao ambao watapenda kusajili kikundi chao, iwe ni Vodacom, Tigo, Airtel au Halotel. Baada ya hapo Mwenyekiti atafuata utaratibu ufuatao kufungua akaunti ya kikundi kidigitali;
AIRTEL KIKOBA.
1. *150*60#
2. Chagua No 6; Huduma za Kifedha
3. Chagua No 3; Airtel Kikoba kisha atafuata maelekezo.
TIGO KIKOBA.
1. *150*01#
2. Chagua No 7; Huduma za Kifedha
3. Chagua No 8; AKIBA kisha No 3, Kikoba na atafuata maelekezo.
M-PESA (M-KOBA).
1. *150*00#
2. Chagua No 6; Huduma za Kifedha
3. Chagua No 3; M-KOBA na atafuata maelekezo.
HALO KIKOBA (Kwa sasa wateja watatumia menu ya benki *150*21#)
1. *150*21#
2. Chagua No 4; Halo Kikoba na kisha atafuata maelekezo
SWALI: KUNA GHARAMA ZOZOTE KUJIUNGA NA KIKOBA KIDIGITALI?
JIBU:
Wakati mwenyekiti anasajili kikundi, ataweka gharama kidogo ya shilingi elfu moja (1,000/=) ambayo itakua kama salio anzia. Baaba ya hapo hakutakua na makato mengine yoyote ya ziada. Aidha, Miamala yote ya wateja kutuma au kwenda kwenye kikundi ni BURE, na miamala yote ya kutoa pesa kutoka kwenye kikundi kwenda kwa mwanachama pia ni BURE. Hakuna MAKATO yoyote.
SWALI: KWANINI MTEJE ATUMIE HUDUMA YA VIKOBA KIDIGITALI?
JIBU:
Ni huduma rahisi inayowezesha wanachama wa Kikundi kufanya shughuli zao kidigtali kwa kupitia simu zao za mikononi bila gharama zozote. Ni salama na inaleta uwazi kati ya wanachama na kikundi kwa ujumla. Kuanzisha kikundi kidigitali ni rahisi kupitia menyu ya mtandao husika kwa simu bila kutembelea tawi la benki au duka la mtoa huduma za simu.
SWALI: KUNA AKAUNTI NGAPI KATIKA HUDUMA YA KIKOBA KIDIGITALI?
JIBU: Kikoba kidigitali inajumuisha akaunti mbili ambazo ni:
- Marafiki / Familia: Hii ni akaunti maalum kwa makundi madogo na yakati, inaweza kuwa familia au marafiki, ujirani mwema, wanadarasa waliosoma pamoja, vikundi vya makanisani au msikitini, vikundi vya vijana, wanawake n.k, wanaokusudia kuchanga pesa kwa lengo maalum na baadaye kuzisambaza kulingana na lengo husika.
- VICOBA / VSLA/SACCOS/YSLA: Hii ni akaunti maalum kwa makundi yenye wanachama wengi na mfumo wa kuuza na kununua hisa, akiba, Michango ya Kijamii na Mikopo.
SWALI: KIKUNDI KINAPASWA KUA NA VIONGOZI WANGAPI?
JIBU: Kila kikundi katika Kikoba kidigitali lazima kiwe na viongozi watatu ambao ni:
- MWENYEKITI: Mwanzilishi na msimamizi wa Kikundi.
- KATIBU: Anaanzisha malipo na mikopo kwa wanachama wengine.
- MWEKA HAZINA: Anathibitisha malipo na mikopo iliyotolewa kwa wanachama.
SWALI: TUNAHAMISHAJE PESA KUTOKA AKAUNTI YA KIKUNDI KWENDA KWA MWANACHAMA?
JIBU: Fedha zitahamishwa kupitia hatua tatu kwenye menyu ya Kikoba kidigitali:
i. Katibu ataanzisha mchakato wa malipo kutoka akaunti ya kundi kwenda kwa mwanachama.
ii. Mweka Hazina atathibitisha malipo.
iii. Mwenyekiti wa kikundi atakubali malipo na fedha zitahamishwa kutoka akaunti
ya kikundi kwenda kwa mwanachama husika.
SWALI: JE, KUNA KIKOMO CHA MIAMALA AU KIASI CHA PESA KWENYE AKAUNTI YA KIKUNDI AU MWANACHAMA?
JIBU: Katika akaunti ya kikundi hakutakuwa na kikomo cha kupokea miamala, lakini kwa mwanachama wa kikundi ataruhusiwa kupokea au kufanya miamala kulingana na kikomo cha miamala cha mtandao wake wa simu.
SWALI: JE, WANACHAMA WA KUNDI KUTOKA MTANDAO MWINGINE, WANAWEZA KUJIUNGA NA KIKOBA KIDIGITALI AMBACHO SIO CHA MTANDAO WAKE WA SIMU?
JIBU: Ndiyo, Kwa kupitia KIKOBA MIX, Huduma ambayo inawaunganisha pamoja kwenye kikoba kidigitali wateja wa mitandao ya Tigo, Airtel na Halotel. Wanachama kutoka mtandao mwingine wanaweza kujiunga na Kikoba kidigitali na wanaweza kuchangia moja kwa moja kwenye kikundi na pia kupokea hela moja kwa moja kutoka kwenye kikundi. KIKOBA MIX inapatikana kupitia menu ya TCB Benki, *150*21# ambapo mteja ataona vikundi vyote vya mitandao tajwa hapo juu.
SWALI: MASHARTI YA CHINI KABISA YA HUDUMA HII YA KIKOBA KIDIGITALI NI YAPI?
JIBU: Kikoba kidigitali lazima wanakikundi wakubaliane wanafungua kikundi chao mtandao gani, na kisha mwenyekiti atafungua akaunti ya kikundi kwenye mtandao husika na kuwaongeza viongozi wengine. Baada ya hapo viongozi wote watatu wataweza kuwaongeza wanachama wote wa kikundi.
SWALI: NANI WA KUWASILIANA NAYE IWAPO KUNA MALALAKIKO, MASWALI, MAPENDEKEZO AU MAOMBI?
JIBU: Mteja ataweza kuwasiliana na huduma kwa wateja wa mtoa huduma za simu kwa malalamiko yoyote, hii inajumuisha kupiga simu 100 au kuwasilisha maswali yao kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya mtandao husika. Pia wateja wanaweza kuwasiliana na TCB Bank huduma kwa wateja kupitia namba +255 787 669 977 na +255 658 767 683 au kutembelea tawi lolote la TCB lililopo karibu naye.